FUNZO KWA MFANO WA P-SQUARE.
Paul Okoye (Mmoja wa Square) vs Anita Okoye (Mke wake).
1. Mkewe alitaka P Square ivunjike ili Paul abaki yake, alifanikiwa.
-Paul alikosea sana, hutakiwi kugombana na mwanaume mwenzako kwa sababu ya mwanamke.
2. Mkewe alimuomba Paul amfanye kuwa director wa kampuni ya Paul (Rudeboy records), Paul alikubali
-Paul anafanya kosa tena kwa kumuhusisha mwanamke na biashara zake, mwanamke hatakiwi hata kujua mshahara wako.
3. Mkewe alimwambia Paul amfukuze kazi meneja wake na amuweke mdogo wake kuwa meneja (mdogo wa mkewe). Paul alikataa.
-Paul alifanya jambo la maana kidogo.
4. Mkewe alitaka kusafiri na Paul kwenye matukio na show zake zote, Paul alikataa.
-Jitahidi usichanganye mapenzi na kazi.,
5. Mkewe aliposikia Psquare inataka kurudi alimkataza Paul kuhudhuria kikao, paul alikataa.
-Kumbuka brothers always comes first.
6. Mkewe alimnyima tendo Paul kwa miezi 5 ili kumuonesha amekasirika. Paul alimuomba mke wa kaka yake Jude aongee na mke wake lakini aligonga mwamba. Paul aliamua kutafuta demu mwingine na kumkodishia nyumba na rasmi akaacha kuomba sex.
-Paul alikuwa mwepesi kuelewa kuwa hapa hamna love nilikuwa natumika na kupoozwa na sex wakati sex zinapatikana kirahisi tu.
7. Mwezi wa 12, mkewe alikataa kuwaruhusu watoto wake kuhudhuria sherehe ya christmas ya ukoo wa Okoye kwenye nyumba ya Jude.
-Kumbuka hutakiwi kulazimisha uwaone watoto, watoto ni wako tu na hakuna kitakachobadilisha hilo, wape matunzo ukiwa mbali na Tunza risiti kuna siku utazihitaji. Narudia (kila malipo Tunza risiti).
8. Mwezi wa 3, mkewe aliomba awapeleke watoto likizo US kwa dada yake mwanamke lakini Paul alimwambia asubiri mpaka August lakini aliwasafirisha bila ruhusa ya Paul.
-Hutakiwi kuvumilia hata kidogo mwanamke asipokusikiliza. Usiwe dick driven wanawake wapo wengi wanaotaka kuishi chini ya amri zako.
9. Mwezi wa 6, Paul alianda surprise kubwa kuwatembelea watoto na mkewe kwenye nyumba ya dada yake USA na akagundua hawapo pale. Ila mwanamke alienda kuishi Utah na ex boyfriend wake.
-Kila siku tunakumbusha Epuka kudate na single mothers, mwanaume aliyemuacha hakuwa mjinga.
10. Paul aliomba kuwaona watoto, lakini alikataa na jamaa akaamua kurudi Nigeria.
-Watoto ni wako kwanini upate tabu kuwaona? Kwa mwanaume Jukumu lake ni kupanda mbegu na kuzimwagilia, hivi Endelea kuwapa matunzo na Tunza risiti ila kamwe
Usilazimishe kawaona, watoto watakutafuta wenyewe au watafute wakishaanza kujielewa.
11. Mkewe alitarajia Paul kuandika talaka lakini mchizi alikaa kimya bila kumsumbua mwanamke, hivi mwanamke aliamua kudai talaka mwenyewe.
-Remain stoic, remain unaffected, usivurugwe hadi avurugwe.
Paul hajawahi kumpiga mwanamke, Paul anampa mwanamke huyo Million 5 kwa mwezi kama matunzo ya watoto.
-Kamwe usipuuzie red flag kwa mwanamke
CREDIT TO OMMYFITNESS.

Comments
Post a Comment