MAMBO 10 AMBAYO MCHEPUKO WA MUMEO UNAFANYA AMBAYO WEWE HUYAFANYI
Kwanini wanaume huchepuka? Hili ni swali ambalo wanawake wengi hujiuliza, hakuna mwanamke anayependa mume wake kuchepuka, ingawa wanawake ni wavumilivu sana katika hili na ni mara chache sana kukuta mwanamke akimuacha mumewe eti kwasababu anachepuka lakini sijawahi kukutana na mwanamke ambaye anafurahia mume wake kuchepuka.
Hakuna sababu maalum ya wanaume kuchepuka, wengi ni ushenzi tu wa tabia, ingawa ni lazima tukubali kuwa wakati mwingine kama ambavyo mume anaweza kumsukuma mkewe kuchepuka, basi hata mwanamke anaweza kumsukuma mumewe kuchepuka. Kuna mambo ambayo mwanaume anayapata kutoka kwa mchepuko ambayo mara nyingi kwa mke hayapatikani na hapa nitayachambua kama ifuatavyo.
(1) Wanashukuru zaidi kwa kidogo kuliko Kulalamikia Kikubwa
Michepuko inatabia ya kushukuru kwa kila kitu inachopata, hata ikipewa hela tu ya Bajaji itashukuru, itaonesha furaha ya wazi. Lakini haiishii katika shukurani ya mdomo tu, lakini pia hutoa shukurani ya kitu kingine. Kwamba mbali ya kumsifia mwanaume, kumshukuru kwa kile alichopewa lakini atataka kumuongezea kitu. Ingawa walipanga kufanya mapenzi siku hiyo, mchepuko utasema “Leo nina furaha sana na nitakupa mambo makubwa” na kweli shughuli ya siku hiyo Kitandani itakuwa pevu.
Mwanamke atajitahidi sana kuonesha shukurani yake kwa vitendo. Hali hii sio tu humfanya mwanaume kutoa zaidi ili kushukuriwa zaidi wakati mwingine lakini pia humfanya kumganda kwani kwa mkewe mara nyingi ni shukurani ya mdomo tu au hakuna shukurani kabisa. Pia baadhi ya wanawake hushukuru kwa kulalamika kwamfano anasema “Nashukuru lakini si ungeleta na kitu flani…” Hii inaboa na kumkatisha mwanaume tamaa.
(2) Hawafanyi kitu kilekile kila siku, Wanawa ‘Surprise’
Hawafanyi kitu kile kile kila siku. Anajua mchepuko wake utamtembelea, labda utapitia ukiwa umetoka kazini umechoka, basi atampikia chakula anachokipenda, ataandaa kitanda vizuri kuliko kawaida, atamuandalia maji yenye viungo au hata kama zawadi flani.
Wanakumbuka vitu vidogo vidogo, kama vile siku za kuzaliwa, kupandishwa cheo na vitu kama hivyo. Watawaandalia visherehe vidogo vidogo hata kama ni vyao wawili na kila siku kutakuwa na kitu kipya. Yaani watawaandalia surprise za kimapenzi hata kama ni kwa mwanamke kuvaa ‘Underwear’ mpya ataifanya kuwa ishu.
(3) Wanajaribu mambo mapya bila kulalamika
Michepuko haina mipaka, sijui mimi sifanyi hiki, oooh hiki sifanyi na kile, wanafanya chochote. Hawafanyi mapenzi kama adhabu au wajibu wao wa kila siku bali kama kitu cha burudani hivyo wakigundua staili mpya watafanya na hata mwanaume akileta staili mpya watajifunza. Badala ya kuanza kuuliza kuwa hili umejifunzia wapi na kuleta maneno maneno wao wapo tayari kujaribu mambo mapya.
Hapa simaanishi kwamba wanafanya kila kitu na haimaanishi wewe njia kuu ufanye kila kitu, lakini kuwa huru kujaribu hasa katika staili. Ila usijaribu yale mambo ambayo yatadhuru afya yako kama kufanya mapenzi kinyume cha maumbile, hakuna mwanaume mwenye akili timamu atakubali kumfanyia mkewe hivyo na akishaanza jua ni rahisi kukuacha akishakuharibu.
(4) Hawalalamikii Mapungufu wanayabeba kama yalivyo
Wanajua hawapo na malaika hivyo wanafurahia kile wanachokipata, inaweza kuwa ni kitandani au katika huduma. Wanapopewa hawalamiki sana. Ingawa kuna vitu vinaweza kuwa haviwaridhishi lakini hawana gubu, hawana kelele za malalamiko hivyo wanaume huona kama ni sehemu ya kupumzishia vichwa vyao hasa kama wake zao ni watu wa kelele sana.
(5) Wanaridhika na kukubali kidogo wanachokipata
Hawapati kila kitu lakini wanaridhika na wanachokipata, wanaridhika na muda mchache wanaokuwa na mwanaume, wanaridhika na matumizi kidogo wanayopewa, wanaridhika na shughuli ya kitandani, hawalalamiki sana na kila wakati wanaonesha furaha na kidogo. Hali hii huwasukuma wanaume kuwahudumia na kuwekeza muda wao kwao zaidi.
Hakuna mtu ambaye anapenda kuhudumia mtu ambaye haridhiki, mtu ambaye kila wakati anataka zaidi. Yaani mwanaume kahangaikia kaleta chakula mezani lakini huridhiki na kuku unataka na samaki, huridhiki na kitenge unataka na Wax. Anachelewa kidogo badala ya kufurahia karudi basi unalalamika kazi nikuchelewa kumbe kachelewa mara moja.
(6) Wanawapa Kipaumbele cha Kwanza na kuonyesha kujali
Wanaweza kuwa na watoto, wana ndugu, wana marafiki lakini michepuko yao ndiyo kipaumbela chao cha kwanza hata kama ni cha kuigiza. Ukipiga simu watapokea na ukiwahitaji watakuwepo, mchepuko unapokuja wanaacha kila kitu na kwenda kusikiliza haja zao.
Wanafanya mambo kwa pamoja, atataka waangalie TV pamoja, atampikia chakula anachotaka sio kile wanachotaka watoto, ataacha marafiki zake na kwenda kumsikiliza na kila wakati atajiweka kuhakikisha anaenda na ratiba ya mchepuko wake. Hajifanyi kuwa bize na kusahau wajibu wake.
(7) Wanafanya Maandalizi ya ndani na nnje
Anajua mchepuko unakuja, atafanya usafi wa kila kitu, kuanzia mwili wake mpaka pale chumbani. Yaani mchepuko ukifika unavuta harufu nzuri na haukutani na kero ndogo ndogo za kuharibu mood. Atapika chakula kizuri na kuandaa kila kitu ambacho mchepuko unapenda.
Atajiandaa kiakili, ataweka matatizo yake pembeni kwaajili ya kumsubiri Mwanaume. Kama ameambiwa atatolewa out basi atajiandaa mapema na kuwa tayari, kwa kifupi mwanaume anapofika kwa mchepuko hukuta kila kitu kiko sawa, mwanamke anavutia na anamaanisha hata kumsogelee.
(
Wanajua wakati wa kulalamika na wakati wa kukaa kimya
Sio kwamba hawalalamiki, sio kwamba hawaombi, lakini wanajua ni wakati gani wa kufanya hivyo. Kabla hajaomba kitu au kulalamikia kuhusu kitu ambacho mwanaume alikifanya na hakikumfurahisha basi hutengeneza mood kwanza.
Watahakikisha kuwa mwanaume hana mawazo na watamhudumia vizuri kabla ya kumlalamikia tena wakiwa wamekaa kimahaba amemlalia kifuani ndiyo anaanza kuongea matatizo yake. Anaongea kwa kubembeleza kama mkia vile, nataka kuonewa huruma zaidi kuliko kulaumu.
(9) Wanasifia hata kama ni uongo lakini wanaigiza vizuri
Wanasifia kila kitu hata kama hawajakifurahia lakini kama wanajua kilifanywa kwa mapenzi basi wanasifia. Lakini pia wanajua matukio muhimu ya wanaume na kuyasifia, amepandishwa cheo, anafanya kazi mpaka usiku badala ya kulalamika husifia ufanyaji kazi wake. Wakati mwingine husifia hata mambo ambayo ni ya kawaida sana, anaweza kusifia hata uendeshaji wa gari wa mwanaume.
(10) Wanawaamini hawachunguzi chunguzi sana
Wao ni michepuko, wanaiba, lakini bado wanawaamini wale wanaume kwamba ni waaminifu. Wakimuona na mwanamke mwingine hawalalamiki sana na wanaridhika na maelezo waliyopewa. Hawahangaiki na simu au kushuku shuku kila kitu. Kuna wanaofikia hatua ya kuanza kuhangaika hawa ni wale ambao washajiona kama wapo kwenye ndoa, ila wengi wanamkubali mwanaume jinsi alivyo na kuamini hivyo hivyo.
(11) Silazima ufanye kila kitu ila jaribu kubadilika
Najua kuna mazingira ambayo wake za watu wanashindwa kuwa kama michepuko. Wala wanawake hamtakiwi kuwa kama michepuko lakini kama kwenye hayo kumi hufanyi hata moja basi ni wakati wa kujiangalia. Unaweza kuwa kila siku unalalamika kuwa mume wangu anachelewa kurudi nyumbani kumbe ana hamu sana ya kuwahi lakini inamlazimu kuchelewa ili kukukwepa wewe.
By plate


Comments
Post a Comment