*ZIJUE ATHARI ZA DHAMBI YA UMALAYA*
*MITHALI 5*
3 Maana midomo ya malaya hudondoza asali,Na kinywa chake ni laini kuliko mafuta;
4 Lakini mwisho wake ni mchungu kuliko pakanga;Ni mkali kama upanga wa makali kuwili.
5 Miguu yake inatelemkia mauti;Hatua zake zinashikamana na kuzimu;
6 Hata asiweze kuiona njia sawa ya uzima;Njia zake ni za kutanga-tanga wala hana habari.
7 Basi, wanangu, nisikilizeni sasa,Wala msiache maneno ya kinywa changu.
8 Itenge njia yako mbali naye,Wala usiukaribie mlango wa nyumba yake.
9 Usije ukawapa wengine heshima yako,Na wakorofi miaka yako;
10 Wageni wasije wakashiba nguvu zako;Kazi zako zikawa ndani ya nyumba ya mgeni;
11 Nawe ukaziombolea siku zako za mwisho,Nyama yako na mwili wako utakapoangamia;
12 Ukasema, Jinsi nilivyochukia maonyo,Na moyo wangu ukadharau kukemewa;
13 Wala sikuisikia sauti ya waalimu wangu,Wala sikuwategea sikio langu walionifundisha!
Bwana Yesu asifiwe sana sana
*Umalaya ni*
Hali ya kukosa uaminifu kwa mume au mke wako ambayo inasababisha mahusiano yaliyoko kati ya mume na mke kuingia dosari.
Pia ni tabia ya kukosa uaminifu moyoni inayompa mtu kuangaika kwenye swala zima la kimahusiano ,Leo unakuta ana huyu ,kesho ana yule mwingine ,hana kikao maalumu ,ni wa kutanga tanga tu kila siku.
Pia *umalaya* ni hali ya kukosa uaminifu kwa Mungu Baba katika Yesu kristo inayompelekea mtu kuangaika kutafuta msaada kwa miungu mingine.Kwa mfano unakuta mtu yupo kanisani na anasema anampenda Yesu lakini kila kukicha anawaendea waganga wa kienyeji wa kila ya miji kutafuta msaada ,hiyo kwa Mungu ni umalaya pia.
Mtu anapokuwa na roho inayomwendesha katika umalaya uwezo wake wa ufanyaji kazi uwa unakaa kwenye kinywa chake ndivyo Mithali 3:5 inenavyo kuwa midomo ya kinywa cha malaya inapokuwa inanena uwa inaachia au inadondosha maneno matamu kama asali na kinywa chake uwa ni laini ili kumlainisha mtu inayemuwinda kwa kufanya nae umalaya ,kama ni miungu migeni uwa inaweka matamanio mazuri sana yenye kushawishi mtu kwenda kuiabudu kinyume na Mungu Baba ,roho hii uwa inapoachia maneno matamu ya kushawishi watu kwa kufanya umalaya ,uwa inawatamanisha mazuri tu ,mambo matamu na aiwapi nafasi ya kufikiri juu ya matatizo ambayo uwapata walionayo mwishoni mwa ufanyaji wao dhambi ya umalaya , aitoi nafasi ya kufikiria juu ya madhara au athari za umalaya ,inaficha madhara yake mpaka pale mtu anapokuja kuharibikiwa.
Uwa haitaki kujulikana kama ni mbaya kwa wanadamu ,inaachia utamu tu ambao umpumbaza mtu anayeufanya asijue kuwa kuna *uchungu mkali* kuliko pakanga na ni mkali kama upanga wa makali kuwili
Mithali 5:4
Mwisho wa umalaya ni mbaya sana ,kwa maisha ya wanadamu ; unapoanza kuufanya Shetani uwa anaweka matamanio ambayo yanafumba macho ya ufahamu wa mtu asione na asijue kuwa anachokifanya ni kibaya sana mbele za Mungu; na kina athari kubwa kwake ,watu wengi uwa wanauliza kuwa uongo wa Shetani ulikuwa upi alipokwenda kwa mkewe Adamu bustanini Edeni ,sikia uongo wake ulikuwa ni huu ,wakati anamwambia ale matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya ,Shetani akumwambia madhara au athari za kula lile tunda bali alimweleza tu uzuri wa kula tu pekee ,akumwambia baada ya kula ni athari gani watapata ,biblia inaeleza kuwa alimtamanisha kwa ujanja wa kigezo cha kuwa kama Mungu ,kufanana na Mungu na mwanamke akayaamini yale maneno matamu na malaini akachuma akala ,usikubali kuliamini kila neno unalolisikia ,lipime kwanza kama ni la Mungu au la ,lina ukweli wa neno la Mungu au la ,Mungu peke yake ndie awezaye kusema ukweli ,Yeye afichi kitu ,aliwaambia kuwa siku mkila mtakufa na kweli walipokula ndipo kifo kikatokea duniani Latino aukuwa mpango wa Mungu watu wafe duniani .
Roho ya umalaya ikikaa kwa mtu uwa inamfanya mtu apende kujipamba kwa uzuri kinyume na yenyewe ilivyo ,yenyewe ni mbaya mno ,haina uzuri inatembea katika mauti ,inakwenda sambamba na roho ya mauti na ya kuzimu ,ikishika mtu inahakikisha inamtembeza mtu kwenye umauti na hatua zake zinaelekea kuzimu akifa tu anelekea kuzimu moja kwa moja
Mithali 5:5
Mauti imo ndani ya umalaya ,na uwa haitaki ijulikane kama imo umo ndani ndio maana uwa inahakikisha mfanya umalaya anajipamba vizuri na kuvutia watu ili iwakamate vizuri na kuwatelemsha mautini na kuzimuni ni kaburi lililopakwa rangi nzuri na chokaa lakini ndani limeoza.
Pia uwa inapofusha macho ya mtu iliyo mnasa asiweze kuona njia vyema ya uzimani ,inamwendesha mtu bila kujitambua na ndio maana mtu akiwa Malaya sana uwa anajiusisha na ushirikina ili kunasa roho za watu na kuziangamiza kuzimu ,unakuta zinatumika dawa za kushikilia waume za watu ,wake za watu ,zinapumbaza akili na fahamu na mtu anajikuta anafanya mambo ya ajabu kabisa ,anasaliti familia au ndoa yake,kama huku kwa Mungu unakuta zinateka mioyo na kuwafanya waache kuabudu Mungu na kuabudu miungu
Mithali 5:6
Dawa ya kuepukana na hii roho ni kuyasikuliza maneno ya Mungu na kuyazingatia moyoni bila kuyaacha
Mithali 5:7
Pia lazima kujitenga na njia zote zenye kufungulia mambo ya umalaya ,tabia za umalaya ,usikaribie mahali popote penye biashara zake na kujiingiza humo ndani kwa sababu ndani ya kazi au shughuli za umalaya kuna upotezaji wa heshima na miaka ya kuishi ,roho au mapepo ya umalaya umfanya mtu apoteze heshima au uthamani wake kwa Mungu na kwa jamii yake kadiri afanyavyo ndivyo na miaka yake inavyozidi kupungua
Mithali 5:9
Jambo lingine baya zaidi ni kwamba uwa unafanya mtu kupoteza nguvu zake za kiafya ,kiuchumi na kimaendeleo ,yaani zinakufilisi ndio maana unakuta mtu anakuwa dhaifu kiroho na kimwili hawezi kufanya vitu vya kimaendeleo kwa sababu ya kunyonywa nguvu zake za kimafanikio ,hapa ndipo wengi upokonywa chota zao za mafanikio yao na kuachwa watupu ,kuna mapepo yanayokaaga ndani ya watu ambao ukijiusisha nao tu kimwili kila kitu kwako utashangaa kinaharibika ,maendeleo yako ya kimwili na kiroho utaona yanakupotea kabisa ,wageni wanabeba kazi zako zote zinakuwa kwa faida yao
Mithali 5:10
Ni hatari sana kwa sababu athari zake pia uenda hadi kwenye uzee wako na pia ukufanya uwe kwenye maombolezo makuu siku yako ya kufariki kwako wakati umelala chini pale kwa ukimwi hapo ndio uwa kuna majuto makuu ,ulipoonywa ulikataa kusikia na ukafanya dharau ,uligoma kukemewa ,ulikataa mafundisho matokeo ni uharibifu mkuu
.jpg)
Comments
Post a Comment