Mmoja ana ndoa 5 mwingine ana 3
Kifupi wote 2 ni miyayusho
Wamekuta wakapiga story wakaona anaenda bora waowane wale raha tu😃
💥Gwiji wa vyombo vya habari, mzee wa miaka 93 amefunga ndoa jana. Hii ni ndoa yake ya tano. Amemuoa Bi Elena Zhukhova mwenye umri wa miaka 63.
Mzee huyu anaitwa Rupert Murdoch. Tajiri wa vyombo vingi vya habari. Kama ulishasikia 'Fox News, New York Post, Washington Journal yeye ndio mmiliki.
Uingereza kuna magazeti makubwa: 'The Times' na 'The Sun'. Yote hayo ni yake. Pia, Murdoch ndiye mwanzilishi wa Sky News.
Bi Elena Zukhova ni mrusi. Alihamia Marekani mwanzoni mwa miaka ya tisini. Hii ni ndoa yake ya tatu. Bi Elena alikuwa mke wa tajiri mkubwa wa mafuta kutoka urusi, bwana Alexander Zhukova. Na walizaa binti anayeitwa Dasha Zhukova.
Dasha Zukhova ndiye yule aliyeolewa na tajiri Roman Abramovich.
©️ Doctor Love

Comments
Post a Comment