⚠️😳🥰 Wanandoa hao wanatarajia kupata mtoto wao wa kwanza hivyo kujawa na furaha isiyoelezeka. Mke huyo anaitwa Cheryl(63) huku mume huyo jina lake likiwa ni Quran(26) hivyo amepitwa miaka 37 na mkewe
Wanandoa hao kutoka nchini Marekani, mtoto wanayetarajia kumpata wamebebewa mimba na mwanamke mwingine waliyemuajiri(surrogate) kwa kazi hiyo tu ya mimba. Mbegu ziliosababisha mimba ni za Quran ila yai ni la mwanamke mwingine ambaye sio Cheryl sababu umri wake tayari umeshayoyoma. Tayari mwanamke waliyemuajiri vipimo vimeonesha ana mimba yao hivyo wanandoa kujawa na furaha sana kwakuwa kipindi cha nyuma walijaribu mara tatu kupata mtoto ikashindikana
Kwa mara ya kwanza wanandoa hao walikutana sehemu waliyokuwa wakifanyia kazi pamoja na kwa wakati huo Quran alikuwa na miaka 15 tu ila hawakuwa wapenzi. 2020 walikutana tena Quran akiwa na miaka 23 na kumfariji Cheryl ambaye alikosoma furaha baada ya kuachia clip mtandaoni akicheza kisha watu kumnanga na kuangua kilio.
Miezi kadhaa baadaye Jamaa huyo alirusha kete kumtongoza mrembo huyo ambapo penzi baina yao likachanua kisha 2022 wakafunga ndoa ambayo ilihudhuriwa na marafiki wao wawili tu, hawakuwaalika watu wengine sababu walikuwa hawalisapoti penzi lao
Kabla hawajakutana, Cheryl tayari alikuwa na watoto 7 aliozaa kutoka mahusiano yake ya awali, pia ana wajukuu 18. Lakini huwa anakutana na mtoto wake mmoja tu na wajukuu wake watatu basi kwakuwa watoto wake wengine sita hawalisapoti penzi lake na Quran kitu ambacho Cheryl anasema kinamuumiza sababu mwanzo watoto wake alikuwa nao karibu sana ila changamoto hawakutaka aolewe na mwanaume huyo aliyempenda hivyo kuwa njia panda
Quran yeye bado hana mtoto, kwahiyo mtoto wanayetarajia kumpata atakuwa wa kwanza kwake ila kwa Cheryl atakuwa mtoto wa nane
Kwenye comments section kuona zaidi video na picha za wanandoa hao wanaopendana kwa dhati

Comments
Post a Comment