WANAWAKE WENGI WANAFELI SANA KWENYE USAFI
Leo acha niwape siri wanawake kuokoa ndoa zao, ukweli mchungu ni kwamba kama kuna jambo linawakera sana wanaume basi huwa ni uchafu wa mwanamke, uchafu wa mwili hususan maeneo ya ikulu(nadhan wakubwa mmenielewa). Maeneo ya barabara na mitaro kuelekea ikulu yanapuuzwa sana, ila ndio yanawakera zaidi wanaume. Kuna wanawake wengi warembo wenye maadili, wengine mpaka na elimu ya kutosha, wengine wajuaji waongeaji kama chiriku wanajua kujipodoa na kuvaa vizuri ila kwenye hili la usafi wa ikulu ni sifuri, zero kabisa. Unakuta wale wadada wa kazi ndio wasafi atar wanazingatia usafi wa ikulu.
Wanaume wengi wanaona aibu kuwaambia hili ila mwisho wa siku wanajikuta wanachepuka kutafuta huduma safi. Mwanamke unapaswa kuwa msafi huko ikulu kuliko hata nyumbani, zingatia sana usafi wa ikulu. Acha kupoteza muda na simu yako au umbea, kumbuka ikulu safi ni ulinzi wa ndoa yako
Kingine wanawake wengi wanachofeli ni kutofanya check up, mwanamke na zama hizi unamalizaje miezi mitatu hujapima u.t.i? Mwanamke unapaswa kujali afya ya ikulu kuliko kitu kingine chochote, unaweza jikuta na vibakteria sugu haufanyi matibabu unaishi na harufu ya sangara alolala
Wanaume wengi sio kwamba hawana nguvu za kiume bali uchafu wanaokutana nao unawatoa mood na kuwamaliza nguvu, wengi wanajikaza tu, AMKENI.
Mwanamke unapaswa kuzingatia kunywa maji mengi na kujiosha vyema ikulu siku zote, ile misitu sio ya kufuga pia waachie kazi hiyo tanapa, unapaswa kuoga angalau mara mbili kwa siku pia na kupaka mafuta yenye kulinda ngozi ya mwili wako.
Kama una changamoto ya harufu sugu au ute mchafu usioeleweka nenda hospitali kubwa na fanya mpango uonane na daktari bingwa wa Wanawake hao wanajua tiba. Unaweza kuta unakunywa ma antibiotic kumbe chanzo cha harufu ni fangasi. Usifosi kujitibu vichochoroni unaweza kuongeza ukubwa wa tatizo au kujipatia madhara makubwa
Binafsi niwape pongezi wanawake wengi wa vijijini usafi huwa wanafundwa kabisa na kuzingatia, bibi zetu vijijini huwa wanawapa mbinu bora sana mabinti kujiweka safi
Mwenye sikio na asikie
Kwenu studio
Comments ziwe fupi fupi leo

Comments
Post a Comment